Uchambuzi wa kitabu cha leading through inflation by Ram Charan
Uchambuzi wa kitabu cha leading through inflation by ram charan. MIKAKATI YA KUENDESHA KAMPUNI WAKATI WA UCHUMI MGUMU, MDORORO NA MFUMUKO WA BEI. Kumhusu Mwandishi Ram Charan ni mshauri wa biashara na uongozi mwenye uzoefu wa muda mrefu wa kufanya kazi na CEO na viongozi wa mashirika mbalimbali. Katika kitabu Leading Through Inflation, anatuelekeza namna viongozi wanavyoweza kuiongoza kampuni wakati wa mfumuko wa bei na mazingira magumu ya kiuchumi. Mazingira kama haya yanahitaji CEO kubadili namna anavyofikiri na kuendesha kampuni. Mikakati iliyokuwa ikifanya kazi wakati wa uchumi mzuri inaweza isitoshe wakati gharama zinaongezeka, nguvu ya fedha ikipungua na wateja kuanza kubadili tabia zao za matumizi. Kwa hiyo, swali si tu: “Tutavukaje kipindi hiki?” Bali pia: “Tunawezaje kuitumia hali hii kuijenga kampuni itakayokuwa imara zaidi baada ya kipindi hiki?” Karibu tujifunze. MAMBO YA KWANZA CEO ANAPASWA KUYAFAHAMU 1. Kubali kwamba mazingira yamebadilika Hatua ya kwanza ni kukubali kwamba kampuni ipo katika mazingira ya mfumuko wa bei na uchumi mgumu. Kukubali hali hiyo hakumaanishi kukata tamaa. Kunamaanisha kubadili mtazamo, mikakati na namna ya kufanya maamuzi ili kuendana na mazingira mapya. 2. Punguza hatari katika mnyororo mzima wa biashara Mabadiliko ya mikakati yanapaswa kuangalia si kampuni pekee, bali pia: Kampuni inaweza kuwa na mpango mzuri lakini ikaanguka kwa sababu mshirika mmoja muhimu katika mnyororo wake ameshindwa kuendelea. 3. Linda fedha taslimu Mfumuko wa bei unaweza kupunguza nguvu ya fedha taslimu na kuongeza mahitaji ya fedha katika uendeshaji wa biashara. Kwa hiyo, CEO lazima awe na uelewa wa karibu wa: Fedha inaingia kiasi gani?Inatoka kiasi gani?Inaenda wapi?Na kampuni inaweza kuendelea kwa muda gani ikiwa mapato yatapungua? Katika kipindi kigumu, cash flow si jambo la kuachia kitengo cha fedha pekee. Ni ajenda ya CEO. MAMBO MATANO YA KUKAZIA MACHO WAKATI WA UCHUMI MGUMU 4. Linda mtiririko wa fedha Kampuni inahitaji kuhakikisha fedha inaendelea kuingia bila kukwama. Hili linaweza kuhitaji: Usiangalie mauzo pekee. Angalia pia mauzo hayo yanabadilika kuwa fedha taslimu kwa kasi gani. 5. Iweke biashara kidigitali Usichelewe kutumia teknolojia katika maeneo ambayo inaweza kuongeza ufanisi. Mifumo ya kidigitali inaweza kusaidia katika: Lengo si kutumia teknolojia kwa sababu ni ya kisasa, bali kutumia teknolojia pale inaposaidia biashara kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. 6. Ondoa vikwazo kwenye mnyororo wa usambazaji Katika mazingira ya gharama zinazopanda, kuchelewa kwa malighafi au bidhaa kunaweza kuongeza gharama zaidi. CEO anapaswa kufahamu wapi kuna vikwazo katika mnyororo wa usambazaji na kufanya kazi kuviondoa. 7. Weka ubunifu karibu na mteja Ubunifu usiwe jambo la kuzungumzia kwenye mikutano pekee. Jiulize: Mteja anahitaji nini sasa?Yuko tayari kulipia nini?Tunaweza kumsaidia kwa namna gani bora zaidi? Hapo ndipo ubunifu unapaswa kuelekezwa. 8. Usipuuze matengenezo Kukwepa gharama za maintenance leo kunaweza kuleta gharama kubwa zaidi kesho. Katika kipindi ambacho fedha ni muhimu, ni rahisi kuahirisha matengenezo ili kuokoa fedha. Lakini baadhi ya matengenezo yanapocheleweshwa, yanaweza kusababisha hasara kubwa zaidi baadaye. USIACHE KUJENGA KESHO 9. Endelea kuangalia wakati ujao Uchumi unapokuwa mgumu, kampuni inaweza kujikuta ikiishi kwa ajili ya kuokoa leo pekee. Lakini CEO anapaswa kuendelea kujiuliza: “Tunataka kampuni hii iwe wapi baada ya miaka kadhaa?” Usiharibu uwezo wa kampuni wa kesho kwa sababu ya changamoto ya leo. MAMBO AMBAYO CEO ANAPASWA KUYAJUA 10. Fahamu namba halisi za biashara CEO anapaswa kuwa na uelewa wa: Usiongozwe na ripoti nzuri kwenye karatasi wakati fedha halisi haipo. 11. Simamia malipo ya wateja Uhusiano mzuri na wateja ni muhimu, lakini kampuni pia inahitaji fedha zake kwa wakati. CEO anapaswa kuwa na mfumo wa kufuatilia madeni ya wateja na kuhakikisha masharti ya malipo yanaeleweka na yanafuatwa. 12. Fanya kazi kwa karibu na CFO CEO na CFO wanapaswa kujadili: CFO anapaswa kuwa mshauri muhimu wa CEO katika maamuzi ya kifedha. MAWASILIANO YA CEO WAKATI WA UCHUMI MGUMU 13. Wasiliana, wasiliana, wasiliana Katika kipindi cha kutokuwa na uhakika, watu huanza kujaza mapengo ya taarifa kwa makisio. Ndiyo maana CEO anapaswa kuwasiliana mara kwa mara. Wafanyakazi wanapaswa kuelewa: 14. Wasiliana kwa uwazi na uzito Mawasiliano ya CEO si kutoa taarifa tu. Ni kuwasaidia watu kuelewa hali halisi na namna wanavyopaswa kuitikia. Usifiche changamoto kwa matumaini kwamba watu hawatajua. Wape ukweli unaohitajika ili waweze kufanya maamuzi sahihi. 15. Pima kama ujumbe umefika Baada ya kuwasiliana, jiulize: Kwanza: Ujumbe umefika kwa watu uliowalenga? Pili: Wameuelewa na wameitikia kwa namna iliyotarajiwa? Tatu: Ni mabadiliko gani ya tabia au utendaji yameonekana baada ya ujumbe huo? Mawasiliano mazuri hayapimwi kwa kusema tu. Yanapimwa pia kwa kile kinachotokea baada ya kusema. 16. Pokea taarifa moja kwa moja CEO anapaswa kuwa na njia za kupata taarifa kutoka kwa watu walio karibu na ukweli wa biashara. Zungumza moja kwa moja na: Usiruhusu taarifa zote zikufikie baada ya kuchujwa na ngazi nyingi za uongozi. 17. Wape watu nafasi ya kusema Zungumza na timu kuhusu: Na muhimu zaidi, tengeneza mazingira ambayo watu wanaweza kusema wanachofikiri bila kuogopa. 18. Waeleze watu kinachoendelea Usidhani kwamba wafanyakazi wanajua hali ya kampuni. Waeleze: “Hivi ndivyo uchumi ulivyo. Hivi ndivyo kampuni yetu ilivyo. Na hivi ndivyo tunavyopanga kukabiliana na hali hii.” Uwazi hujenga uelewa na uwajibikaji. 19. Tafuta wawekezaji sahihi CEO anapaswa kujenga mahusiano na wawekezaji ambao wanaelewa biashara na wanaweza kuendelea kuunga mkono kampuni katika mazingira magumu. MAUZO NA UPANGAJI WA BEI WAKATI WA MFUMUKO WA BEI 20. Bei lazima iendane na soko Upangaji wa bei haupaswi kufanywa kwa hisia. Angalia: 21. Usichelewe kupandisha bei unapolazimika Gharama zinapopanda, kuchelewa kurekebisha bei kunaweza kuendelea kula faida ya kampuni. Kabla ya kupandisha bei, fahamu: Kama wateja hawakubali bei mpya, usikimbilie kudhani kwamba suluhisho ni kurudi tu kwenye bei ya zamani. Fanya utafiti. Chunguza soko. Pitia gharama. Kisha tengeneza mpango unaowezekana. 22. Si kila mteja ni mteja sahihi Kauli kwamba “mteja ni mfalme” haimaanishi kwamba kila mteja anapaswa kubaki kuwa mteja wa kampuni kwa gharama yoyote. CEO anapaswa kujua: Ni wateja gani wanaongeza thamani?Ni wateja gani wanatumia rasilimali nyingi kuliko thamani wanayoleta? Katika mazingira magumu, uteuzi wa wateja unakuwa muhimu zaidi. 23. Wafahamu washindani Jua: Na unapobadilisha bei, mteja anapaswa kuelewa thamani inayosababisha mabadiliko hayo. 24. Usichanganye ukuaji na afya ya biashara Kampuni inaweza kukua kwa mauzo lakini ikawa inazalisha cash flow dhaifu. Kwa hiyo usiangalie: “Tumekua kwa asilimia ngapi?” Angalia
Uchambuzi wa kitabu cha leading through inflation by Ram Charan Read More »

