Wiki hii tumeshuhudia historia kubwa: Mfanyabiashara mkubwa wa Tanzania, *Bwana Rostam Azizi, amenunua *asilimia 54.08% controlling stake katika Nation Media Group (NMG) – moja ya kampuni kubwa zaidi ya magazeti, TV na vyombo vya habari nchini Kenya. Hii ni hatua ya kihistoria na inaonyesha kuwa WaTanzania wanaweza na wanapaswa kuwekeza moja kwa moja Kenya na EAC. Mtazamo wangu ni kwenye uono wa biashara na uwekezaji.

Pamoja na hilo lakini hii inatufanya tujiulize maswali magumu kulingana na data (kutoka ripoti za EAC, TIC, BOT ):

  1. Biashara ndani ya EAC bado ni ndogo mno. Mwaka 2017 ilikuwa chini ya 10% tu. Leo (2025/2026) imefikia karibu 12–15% pekee ya biashara yote ya EAC. Ikilinganishwa na:
    SADC: ~22–25%
    EU: ~65–68% Hii inamaanisha bado tunauza zaidi nje ya Afrika kuliko sisi kwa sisi.
  2. *Kampuni za Kenya nchini Tanzania: Zipo karibu 529, zimewekeza zaidi ya *$1.8 Bilioni (karibu TSh 5 trilioni) na zimeajiri zaidi ya Watanzania 56,000. (Hizi ni data ya 2025–2026).
  3. *Kampuni za Tanzania nchini Kenya: Zipo *karibu 30 tu (au kidogo zaidi katika miradi mikubwa kama Amsons na Taifa Gas). Pengo la usawa ni kubwa sana!

Ni sahihi kusema Bwana Rostam Azizi ameonyesha njia nyingine badala ya kungoja Kenya ije tu, tunaweza kuenda na kuwekeza Kenya na EAC?

Swali kwa mjadala wetu leo:

Nini maoni yako?